MAKUBALIANO YA VIGEZO NA MASHARTI 

Vimesasishwa tarehe 01-09-2023 
  
Vigezo Kwa Ufupi 
  
Kwa kupakua na kutumia aplikeshini yetu, unathibitisha kukubaliana na kufungwa na masharti ya huduma yaliyopo hapo chini kwenye Vigezo na Masharti. Masharti haya yatatumika katika aplikesheni pamoja na njia nyingine yeyote ya mawasiliano kati yako na Zanzicab kama vile barua pepe. 
Zanzicab haitawajibika namna yeyote, iwe moja kwa moja au la, mahususi, bahati mbaya au uharibifu wowote utakaojitokeza, ikiwa pamoja, lakini bila kikokomo, upotevu wa taarifa au hasara, itakayotokana na kutumia au kushindwa kutumia aplikesheni, hata kama Zanzicab au mwakilishi wake ametaadharishwa kuhusu uwezekano wa uharibifu huo. Kama matumizi yako ya aplikeshini yatalazimisha marekebisho, uboreshwaji au masahihisho ya kifaa chako au data, utahusika pekee na gharama zozote zitakazojitokeza. 


Zanzicab haitahusika na matokeo yeyote yanayoweza kutokea katika kutumia aplikesheni. Tunahifadhi haki ya kufanya mabadiliko ya bei na kubadili masharti ya matumizi muda wowote.  
  
Kibali 

Zanzicab inakupa kibali kinachoweza kutenguliwa, kisichokuwa wazi, kisichohamishika, chenye kikomo , cha kupakua, kusakinisha na kutumia aplikesheni kwa mujibu wa makubaliano haya. Vigezo na Masharti haya ni mkataba baina yako na Zanzicab(“sisi”, “yetu “, “tu..”). 
 
Ufafanuzi na maneno muhimu
 
Kwa Vigezo na Masharti haya: 

  • Kampuni: Tunapotaja neno “kampuni”, “sisi”, “yetu”, “tu..’’ inamaanisha Zanzicab ina wajibika kwa taarifa zako chini ya Kanuni za Faragha. 

  • Nchi: Ambapo dereva wa Zanzicab anaishi, tukimaanisha Tanzania. 

  • Mteja: inamaanisha mtu ambaye anaridhia kutumia huduma ya Zanzicab Driver kama dereva.

  •  Kifaa: chombo chochote cha kielektroniki kama simu janja, tableti, kompyuta au chombo kingine chochote kitakachotumika ambapo aplikesheni ya Zanzicab Driver imesakishwa na kinatumika kufikia huduma zake. 

  • Anuani ya IP: Kila kifaa kinachounganishwa kwenye mtandao wa Intaneti upatikwa namba ifahamikayo kama namba ya anuani ya protokali ya intaneti au anuani ya IP, ambayo mara nyingi hutumika kutambua mahali ambapo kifaa kinachounganisha kwenye Intaneti kipo. 

  • Mfanyakazi: Watu ambao wameajiriwa na Zanzicab au wanatoa huduma kwa mkataba kwa niaba ya Zanzicab 

  • Taarifa binafsi: Taarifa zozote ambazo moja kwa moja au la, au zinapounganishwa na taarifa nyingine, ikiwa pamoja na namba ya utambulisho binafsi (PIN) - zinaweza kutumika kumtambua mtu halisi. 

  • Huduma: inamaanisha huduma ambazo zinatolewa na Zanzicab Driver, kama zilivyobainishwa kwenye vigezo na masharti katika jukwaa hili. 

  • Tovuti: Tovuti ya Zanzicab inayopatikana katika anuani: zanzicab.com 

  • Wewe: mtu unayejiandikisha na Zanzicab Driver kutumia huduma zake. 


 
Ukomo 

Unaafiki hutofanya na hautoruhusu wengine

  • Kutoa leseni, kuuza, kuazimisha, kukabidhi, kusambaza, kuhamisha, kushirikisha, kufungua au namna yeyote ile kujinufaisha kibiashara kwa kutumia huduma hii. 

  • Kubadilisha, kutengeneza aplikesheni kama hii kwa kuigiza, kuivunja vunja, kufichua mfumo wa siri, kutaka kufahamu namna sehemu yeyote ya aplikesheni inavyofanya kazi kwa lengo la kutengeneza aplikesheni kama hii. 

  • Kuondoa, kubadili au kuzuia kuonekana kwa notisi ya umiliki (pamoja na notisi ya haki miliki au chapa biashara) 


Ridhaa yako 

Tumesasisha vigezo na masharti yetu kukupa uwazi kamili nini vya kuzingatia unapotumia huduma yetu. Kwa kutumia huduma yetu, kuandikisha akaunti, unaridhia kukubaliana na Vigezo na Masharti yetu. 
 
Mabadiliko kwenye Kanuni na Masharti yetu 

Wewe unatambua na kukubaliana kwamba tunaweza kusimamisha (kwa kudumu au kwa muda mfupi) utoaji wa huduma (au kipengele chochote katika huduma) kwako au kwa watumuaji wote kwa ujumla muda wowote, bila kutoa taarifa kwako kabla. Wewe unaweza kuacha kutumia huduma muda wowote. Wewe hauhitaji kutupa taarifa unapositisha kutumia huduma yetu. Wewe unatambua na kukubaliana kwamba kama tukikuzuia kutumia akaunti yako, unaweza pia kuzuiliwa kufikia huduma yetu, taarifa zako au mafaili yeyote au vitu vingine vyovyote ambavyo vimo ndani ya akaunti yako. Kama tukiamua kubadilisha Vigezo na Masharti, tutatangaza mabadiliko hayo kupitia ukurusa huu wa tovuti, na/au kusasisha tarehe ya Vigezo na Masharti hapo juu. 
 
Mabadiliko katika Huduma Yetu 

Tunahifadhi haki ya kufanya mabadiliko, kusimamisha au kutoendeleza, kwa muda mfupi au kwa kudumu, huduma hii au huduma nyingine yeyote ambapo inaunganishwa, kwa kutoa au kwa kutotoa taarifa na bila kuwa na dhima kwako. 
 
Kusasishwa kwa Huduma Yetu 

Tunaweza, kila inapohitajika, kufanya maboresho kwenye vipengele au aina ya matumizi ya huduma yetu, ikiwa pamoja na viraka, marekebisho ya makosa, kusasisha, matoleo mapya na mabadiliko mengine(“Usasisho”). Mabadiliko kwenye aplikesheni yanaweza kubadili au hata kufuta vipengele na/au aina za matumizi ya huduma yetu. Unaafiki kwamba hatuna jukumu kwako (I) kufanya maboresho yeyote, or (ii) kuendeleza au kuwezesha kipengele chochote na/au aina ya matumizi ya huduma kwako. Kadhalika unaafiki kwamba maboresho yote yatakuwa (i) ni sehemu ya msingi ya huduma hii, na (ii) Vigezo na Masharti haya yataendelea kutumika baada ya maboresho hayo. 
 
Muda wa Matumizi na Ukomo 

Makubaliano haya yatabaki yanatumika mpaka pale yatakapokatishwa na sisi au wewe. Tunaweza, kwa matakwa yetu binafsi, muda wowote na kwa sababu yeyote, kusimamisha au kusitisha haya makubaliano kwa kutoa au kutokutoa taarifa kabla. Makubaliano hayo yatasita papo hapo, bila taarifa kabla kutoka kwetu, iwapo utashindwa kufuata kanuni yeyote katika Makubaliano. Wewe pia unaweza kusitisha makubaliano haya kwa kufuta kabisa aplikesheni yetu na vivuli vyake vyovyote kutoka katika kifaa chako. Kusitishwa kwa makubaliano haya hakutaondoa haki zetu au uwezo wetu wa kisheria au kwa usawa iwapo kanuni zilivyunjwa na wewe (wakati makubaliano yanatumika) katika yeyote ya majukumu yako kwa mujibu wa Makubaliano ya sasa. 
 
Fidia 

Unakubali kutufidia na kwamba sisi, kampuni mama yetu, matawi yetu, washirika wetu, maofisa wetu, wafanyakazi wetu, wawakilishi wetu na wanaotupatia leseni (kama wapo) hatutoingia katika gharama yeyote kutokana na madai, ikiwa pamoja na ada za mawakili, yaliyosababishwa au kutokana na wewe: (a) kutumia huduma hii; (b) kuvunja makubaliano haya au sheria au kanuni; au (c ) au kuvunja haki za mtu yeyote wa tatu. 
 
Hamna Dhamana 


Huduma hii inatolewa kwako “KAMA ILIVYO” na “INAVYOPATIKANA” pamoja na makosa na mapungufu bila dhamana ya aina yeyote. Kwa kadri inavyoruhusiwa katika sheria, sisi, kwa niaba yetu binafsi na kwa niaba ya washirika wetu na watupatiao huduma, tunakana dhamana yeyote, iwe imeelezwa wazi, imesadikiwa, kisheria au namna yeyote, kuhusu huduma yetu, ikiwa pamoja na dhamana kwamba inafaa kwa biashara, inafaa kwa lengo lolote maalum. Bila kikomo cha maelezo yaliyotangulia, hatutoi dhamana au kujifunga, na hatufanyi madai kwamba huduma yeyote itakidhi mahitaji yako, kukupatia matokeo uliyokusudia, kushabihiana au kufanya kazi pamoja na aplikesheni nyingine, tovuti, mfumo au huduma nyingine, kufanya kazi muda wote bila kukata mawasiliano, kufikia kiwango chochote cha utendaji au uhakika wa kufanya kazi au kufanya kazi bila makosa au kwamba makosa au mapungufu yanaweza ama yatarekebishwa. 
 
 
Kikomo cha Dhima 

Bila kujali hasara yoyote unayoweza kupata, dhima kwetu na kwa wasambazaji wetu chini ya kifungu chochote katika makubaliano haya, itakoma kwenye kiwango cha pesa ulicholipa ili kutumia huduma hii. Kwa kadri inavyoruhusiwa na sheria, kwenye tukio ambapo sisi au wasambazaji wetu wanajibika kwenye uharibifu wowote wa moja kwa moja au vinginevyo (pamoja, lakini sio mwisho, uharibifu kwa kupoteza faida, kwa kupoteza data au taarifa zingine, kwa biashara kusitishwa, kwa majeraha ya mwili, kwa upotezu wa faragha unaotokana na au kwa namna yeyote unahusiana na kutumia au kushindwa kutumia huduma hii, aplikesheni ya mtu mwingine na/au kifaa cha mtu mwingine kilichotumika pamoja na huduma hii, au kwa mujibu wa kifungu chochote cha makubaliano haya), hata kama sisi au msambazaji wetu yeyote ametaarifiwa kuhusu hasara hiyo na hata kama huduma imeshindwa kwenye lengo lake la msingi. 
 
Utengano 

Kama kifungu chochote cha makubaliano haya kitaonekana hakitekelezeki au batili, kifungu hicho kitabadilishwa na kutafsiriwa ili kufikia malengo ya kifungu hicho kadri iwezekanavyo chini ya sheria na vifungu vilivyobaki vitaendelea kutumika kikamilifu. 
Makubaliano haya, pamoja na Kanuni za Faragha na notisi nyingine zozote za kisheria zilizochapishwa na sisi kwenye huduma hii, zitakuwa ni sehemu ya makubaliano kamili kati yetu na wewe kuhusu huduma hizi. Ikiwa vifungu vyovyote vya makubaliano haya vitakuwa batili kwa mujibu wa sheria, ubatili wa vifungu hivyo hautaathiri uhalali wa vifungu vilivyobakia katika makubaliano haya, ambavyo vitaendelea kutumika kikamilifu. Hakuna msamaha wa kanuni yeyote katika Makubaliano haya ambao utachukuliwa kama wa kudumu kwa kifungu hicho au kingine chochote, na sisi kutotumia haki yetu au kifungu katika haya makubaliano haina maana haki ya kifungu hicho imeondolewa. WEWE NA SISI TUNAKUBALIANA KWAMBA HATUA ZOZOTE ZITOKANAZO AU ZIHUSIKAZO NA HUDUMA YETU LAZIMA ZIANZE NDANI YA MWAKA MMOJA (1) BAADA YA SABABU KUBAINISHWA. VINGINEVYO HATUA KAMA HIYO HAITATEKELEZWA KABISA. 
 
Msamaha 

Isipokuwa kama ilivyoelezwa humu, kushindwa kutumia haki au kuhitaji utekelezaji wa jukumu chini ya makubaliano haya hakutaathiri uwezo wa yeyote kati yetu kutumia haki hiyo au kutaka utekelezaji kama huo muda wowote baadaye, kadhalika msamaha wa kuvunja kifungu hautamaanisha kwamba msamaha huo utaendelea kufaa kama kifungu kitavunjwa tena. 
Kutotumia, na kuchelewa kutumia haki au nguvu na upande wowote katika makubaliano hakutamaanisha kwamba haki hiyo au nguvu hiyo haipo tena. 
 
Kusasishwa kwa Vigezo Vyetu 

Tunaweza kubadilisha huduma na kanuni zetu, na tunaweza kuhitaji kufanya marekebisho ya Vigezo hivi ili viendane na huduma na kanuni zetu kwa usahihi. Isipokuwa inapotakiwa na sheria, tutatoa taarifa (kupitia kwenye huduma yetu) kabla ya kufanya mabadiliko ya vigezo hivi na kukupa wasaa wa kuvipitia kabla havijaanza kutumika. Hivyo, kama utaendelea kutumia huduma, utafungwa na vigezo vipya. Kama hutaki kukubaliana na hivi au mabadiliko mengine ya vigezo unaweza kufuta akaunti yako nasi. 
 
Miliki 

Jukwaa letu na vyote vilivyomo, vipengele na matumizi (ikiwa pamoja, lakini bila kuishia taarifa zote, programu, maandishi, maonyesho, picha, video na sauti, muundo, uchaguzi na mipingalio yake), vinamilikiwa na sisi, watoaji wa leseni au walioweka nyenzo kama hizo na zinalindwa na sheria za Tanzania na za kimataifa za hakimiliki, alama za biashara, patenti, siri ya biashara na miliki zingine au sheria za haki za umiliki. Nyenzo haziwezi kutengenezwa vivuli, kurekebishwa, kutengenezwa tena, kupakuliwa ua kusambazwa namna yeyote, kijumla au kwa vipande, bila ya kuwa na ruksa ya kimaandishi iliyotolewa kabla na sisi, isipokuwa na kama tu ilivyoainishwa katika Vigezo na Masharti haya. Matumizi yeyote ya nyenzo bila idhini yanakatazwa. 
 
Promosheni  

Tunaweza, kila itakapofaa, kuweka maudhui, promosheni, bahati nasibu au vivutio vingine ‘promosheni’ ambavyo vitakuhitaji utume viambatanisho au taarifa kukuhusu. Tafadhali jua kwamba promosheni zote zitaendeshwa na kanuni tofauti ambavyo vinaweza kuwa na kanuni fulani fulani za mahitaji ili kushiriki, mathalani vikwazo vya umri au sehemu ya nchi alipo mshiriki. Utawajibika kusoma kanuni zote za promosheni kufahamu kama au la unaruhusiwa kushiriki. 
 
Kanusho 

Hatuhusiki na maudhui yeyote, maandishi au mionekano mingine yeyote. Hatutoi dhamana au uthibisho wa manufaa. Hakuna mazingira ambapo tutahusika kwa hasara au hasara yoyote, maalum, ya moja kwa moja, iliyosababishwa au iliyojitokeza yenyewe au uharibifu mwingine wowote ule, uwe ni kutokana na uzembe au vinginevyo, unaotana na au unaounganishwa na matumizi ya huduma au vilivyomo katika huduma. Tunahifadhi haki ya kufanya nyongeza, kuondoa, au kubadilisha maudhui katika huduma muda wowote bila kutoa taarifa kabla. 
Bei na taarifa za upatikanaji zinaweza kubadilika muda wowote bila ya taarifa. Bila kujifunga na yaliyotajwa kabla, hatutoi dhamana kwamba huduma yetu itapatikana bila kukatika, bila kuvurugika, kupatina kwa wakati, au kutokuwa na makosa. 
 
Mawasiliano 
 
Usisite kuwasiliana nasi kama una maswali yeyote 

  • Kwa barua pepe: info@zanzicab.com 

  • Kwa simu: +255 (0) 756 448 873  

  • Pia unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia kwenye App ya Zanzicab