Tunaomba rukhusa zifuatazo kwa ajili tu ya kuwezesha aplikesheni kufanya kazi kwa usahihi. Jua kwamba hatuhifadhi taarifa zozote zinazotambulisha watumiaji wetu.
android.permission.CAMERA: Kamera hutumika kwa ajili ya kuchukua picha yako na chombo chako na vitabulisho vyako kwa ajili ya uhakiki wakati wa kujiandikisha. Hakuna matumizi zaidi ya hayo.
android.permission.READ_PHONE_STATE: Taarifa hii inahitajika ili kufahamu kifaa chako kipo katika hali gani wakati aplikesheni inatumika.
android.permission.GET_ACCOUNTS: Taarifa hii inaweza kutumika kwa ajili ya kutambua akaunti ya Google inayotumika.
android.permission.READ_CONTACTS: Taarifa za orodha ya mawasiliano zinaweza kuhitajika ili kupiga simu ya dharura kupitia aplikesheni.
Taarifa zinazopatikana kupitia rukhusa hizi zinahifadhiwa kwa umakini wa hali ya juu na kwa kufuata miongozo ya rukhusa ya Google.
ACCESS_FINE_LOCATION
ACCESS_COARSE_LOCATION
ACCESS_BACKGROUND_LOCATION
ACCESS_FINE_LOCATION & ACCESS_COARSE_LOCATION:
Rukhusa hizi zinatuwezesha kukufikia mahali ulipo kwa ajili ya kutoa huduma yetu. Tunatumia huduma za mahali kwa kufuata kanuni za Google kwa watengeneza programu. Hatutampatia mtu au chombo chochote taarifa za mahali au taarifa za mteja kwa lengo lolote lile. Faragha yako ndio jambo la muhimu zaidi na taarifa hizi zinatumika kwa usalama na kukidhi vigezo vya usalama vya Google.
ACCESS_BACKGROUND_LOCATION:
Rukhusa hii inatumika ili kuwezesha kufuatilia mwenendo wa safari, kwa kufuata miongozo ya Google Play kwa watengenezaji wa programu. Kama ilivyo na taarifa nyingine za mahali, hatutamshirikisha mtu yeyote wa tatu na taarifa hizi.
Tunathamini mrejesho wako kuhusu namna tunatunza faragha, na unaweza kutuma maoni yako kufuata maelekezo ya mawasiliano katika aplikesheni yetu. Kama una dukuduku lolote kuhusu Kanuni za Faragha hizi, tupo tayari kusikia na ikiwezekana kuyafanyia kazi pale hali ya gharama au muda itakaporuhusu. Tafadhaili jua kwamba tunaweza kusasisha Kanuni hizi kila itakapohitajika, na kuwa huru kuwasiliana nasi iwapo una maswali au dukuduku.
AINA YA TAARIFA TUNAZOKUSANYA
Wakati unatumia huduma yetu, tunaweza kuomba kupata taarifa zinazoweza kukutambua kwa ajili ya mawasiliano na uhakiki. Hizi zinaweza kuwa:
Barua pepe
Jina la kwanza na la mwisho
Namba ya simu
Anuani, Mkoa, Mji, postikodi
Taarifa za matumizi
Ujumbe mfupi wa maneno – kwa ajili ya uhakiki
Rukhusa ya ujumbe mfupi wa maneno inahitajika kwa ajili ya uhakiki wa namba yako ya simu unapoingia kwenye aplikesheni ili kuhakiki utambulisho wako.
Wakati unatumia aplikesheni, kwa kutumia rukhusa ya hapo awali, tunaweza kukusanya:
Taarifa ya mahali ulipo
Taarifa ya orodha ya mawasiliano kwenye simu yako
Taarifa zinaweza kuhifadhiwa katika kompyuta zetu au kwenye kifaa chako, na unao uwezo wa kuzuia au kuwezesha kufikiwa kwa taarifa hizi muda wowote utakapohitaji kupitia kwenye mipangilio ya simu/kifaa chako. Kumbuka tu kwamba aplisheni yetu inaweza kushindwa kufanya kazi ipaswavyo iwapo utazuia taarifa hizi kufikiwa.
Taarifa zifuatazo za matumizi hukusanywa moja kwa moja unapotumia huduma yetu
Anuani ya IP ya kifaa chako
Aina na vesheni ya kivinjari unachotumia
Kurasa utakazotembelea
Tarehe na muda wa kutembelea
Muda uliotumika katika kurasa wakati imetembelewa
Vitambulishi vya kipekee na taarifa za uchunguzi za kifaa chako
Unapotembelea huduma yetu kupitia kwenye simu ya mkononi, tunaweza kukusanya taarifa zaidi kama vile aina ya kifaa, Kitambuisho pekee, anuani ya IP ya mtandao, programu ya uendeshaji ya kifaa, aina ya brauza na taarifa nyingine za uchunguzi.
Tafadhali jua kwamba pia tunakusanya taarifa zinazotumwa na brauza yako kila unapotembelea huduma yetu au unapoifikia kupitia kwenye kifaa cha mkononi.
Kwa kutumia aplikesheni yetu au huduma yetu, unakiri kwamba umesoma na kukubaliana na vigezo vilivvyoainishwa kwenye hizi Kanuni za Faragha. Faragha yako ni muhimu sana kwetu na tunajitolea kulinda usalama wa taarifa zako.